Latest News 27 May 2019

News Images

AGIZO LA AFISA MTENDAJI MKUU KWA KANDARASI WA MELI MPYA Z.VICTORIA

Afisa mtendaji mkuu Kampuni ya Huduma za Meli nchini Ndugu Eric Benedict HamissiAmeagiza uingizwaji Conteiner za Vyuma vitakavyotumika kujengewa Meli mpya vipitie katika Bandari yetu ya Dar –es – salaam na pia Reli yetu ya kati hadi Mwanza na si njia nyinginezo.

Amesema hakuna sababu yoyote ya kupindisha hilo kwani Bandari yetu inauwezo wa kuhimili mzigo huo kwa wakati na pia Reli yetu inauwezo wa kufikisha mzigo huo Mwanza kwa wakati.

Jumla ya container mia tatu(300) zenye ukubwa wa futi 40 zinataraji kuanza kuingia nchini kati ya mwezi August Mwishoni na September.

Ameyazungumza hayo katika kikao cha Pamoja kati ya Mkandarasi kutoka Korea Kusini Gas Entec ambaye ndiye mjenzi wa Meli hiyo Mpya ambayo tayari inaakisi jina la mh. Rais Magufuli (Meli ya Magufuli) walipokuwa Mwanza kwa mara ya kwanza katika ukaguzi wa sehemu itakapojengewa Meli hiyo.

Hii ilikuwa ni hatua ya tatu ambapo tayari ujenzi wa Meli hiyo ulishaanza nchini Korea ya Kusini kwa hatua ya kwanza ya Michoro ambayo ilikamilika na kupitishwa na Jumuiya ya Kimataifa inayosimamia viwango vya ujenzi wa Meli Duniani (Lloyd Registry-UK) na pia kuthibitishwa na Wataalamu wa Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania.

Hatua ya pili ilikuwa ni ukataji vyuma vya meli na uagizaji vifaa muhimu kama Injini kutoka kwa watengenezaji mashuhuri wa vifaa hivyo Duniani. Awamu iliyoanza mwezi May 2019 na itakamilika katikati ya mwezi Jun 2019 ambapo vifaa vyote sasa vitakuwa tayari kusafirishwa.

Baada ya kuwasili vifaa vyote vinavyohitajika, ambavyo vinataraji kufika kati ya mwezi August na September 2019 utekelezaji wa uunganishaji vyuma utaanza na hapo utachukua miezi 12.

Meli hii inataraji kukabidhiwa September 2019