Latest News 24 Jun 2019

News Images

KIKAO CHA AFISA MTENDAJI MKUU KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI NA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI HIYO

Kikao cha Afisa mtendaji mkuuKampuni ya Huduma za meli nawafanyakazi wa kampuni hiyo mapema tarehe 24/06/2019 kutathmini utendaji kazi lakini pia kukumbushana majukumu ya kila mfanyakazi kwa manufaa ya kampuni

Katika kikao hicho, Afisa mtendaji amewashukuru wafanyakazi kwa ushirikiano wanaompa hadi sasa kwani ndio unaochochea mafanikio ya kampuni

Amesema kipimo kikubwa cha uwajibikaji na uaminifu kwa serikali iliyotuamini na kutupa pesa za kufufua kampuni hii ni utekelezaji wa maazimio yote kwa asilimia zote.

Ametolea mfano Usimamizi wa Miradi mikubwa inayoendelea sasa, kwamba iwapo itakamilika kinyume na matarajio,kwa maana ya mapungufu kwa baadhi ya sehemu.. hiyo itakuwa ni doa kubwa na litaondoa hali ya uaminifu tunaopata au tulio nao sasa.

‘’Mheshimiwa rais alituamini na kutupa nafasi tena kwa maana ya kututoa huko tulipo kuwa, Juzi Mheshimiwa Waziri Kamwelwe mmemsikia alipoongea nasihapa kaeleza matarajio yake kwetu.. sasa kwanini tuwaangushe watu hawa?... Alisema Eric’’ Nawaomba tushikamane na tufanye kazi kwa ushirikiano zaidi lengo letu liwe moja tu..Kuifanya kampuni kusimama upya kama malengoya mh.rais yalivyo

Binafsi nimeamuakujitoa kwaajili yenu ilitufikie malengo ambayo mungu akisaidia uhai tutaenda hadi Baharini mda si mrefu kwa kuwa na meli yetu huko.

Nao wafanyakazi wa kampuni ya Huduma za meli wamemshukuru Afisa mtendaji mkuu kwa jitihada zake za kuwapigania na hadi serikali kuona umuhimu wa kuwalipa mishahara yao waliyokuwa wakidai,lakini kubwa pia hivi karibuni serikali imewapa pesa ya kulipwa kwa wakati kwa muda wa miezi 27

Pamoja na Shukrani lakini pia wamezungumzia baadhi ya matatizo yao ambayo wangeomba yatatuliwe ambapo yote yamejibiwa na mengine uongozi umeyachukua na kuahidi kuyafanyia kazi kwa haraka.