Latest News 06 Sep 2019

News Images

MAFANIKIO MWAKA MMOJA USHOROBA WA KATI, UGANDA KUFUFUA BANDARI YA JINJA

Mafanikio(Ushoroba wa Kati) njia ya usafirishajimizigo kwanjia ya Bandari,Reli na Maji kwa maana ya Z.Victoria kuelekea nchini Uganda na hatimaye Sudan ya Kusini yameongezeka ambapo mara hii kupitia Shirika la chakula Duniani WFP na wadau wa safari hii ambao ni Tanzania na Uganda wamefanya Ziara katika Bandari ya Jinja nchini Uganda kuona uwezekano wa kuongeza Bandari ya kupitishia Mizigo.

Wakiwa Jinja nchini Uganda, Wakuu wawakirishi wa Mamlaka za Bandari,Kampuni ya Huduma za Meli pamoja na Shirika la Reli nchini Tanzania na Uganda , wawakirishi wa Shirika la Chakula Duniani WFP wamekubaliana kufanya marekebisho katika Bandari ya Jinja ili kuongeza wigo wa upitishaji Mizigo lakini pia kutanua njia ya Biashara katika ukanda wa Nchi za Afrika Mashariki.

Nchi ya Uganda inategemea Bandari mbili ambazo ni Port Bel na Jinja .

Ni miaka zaidi ya kumi sasa Bandari hii ilikuwa imesimama bila kufanya shughuli yoyote kitendo kilichopelekea kun’golewa kwa baadhi ya miundo mbinu yake inayokadiriwa kama kilomita nne kutoka Stesheni ya Jinja.