Latest News 08 Jan 2020

News Images

MATEGEMEO YA MV.VICTORIA KATIKA HATUA ZA MWISHO UKARABATI KABLA YA KUREJEA SAFARI ZAKE

Hatimaye Meli ya MV.Victoria ambayo ni kipenzi cha wana Kanda ya Ziwa ambayo pia Imebeba Jina la Ziwa husika, imefikia katika hatua nzuri naya mwisho kuelekea hitimisho la ukarabati wake.

Katika hatua za Mwanzo za Ukarabati wake, Ilipandishwa katika Chelezo kwa hatua ya Kwanza ya ukaguzi wa chini ya mwili wa Meli na baada ya hapo ikashushwa na kuanza kufanyiwa shughuli ya usafi wa ndani, kwa maana ya kutolewa vifaa vyote chakavu na kuondoa rangi yote ya zamani pamoja na kukata sehemu zote za bati(Plates) ambazo zilionekana kuisha ubora wake.

Baada ya hapo ilipandishwa tena katika Chelezo ili kuangaliwa tena uhai wa mwili wake chini ya meli ambapo zipo sehemu zilizorekebishwa tena kama sehemu ya eneo la mizigo ambapo zipo sehemu zilizobadirishwa bati zake kwa sehemu kubwa kwani zilionekana kuisha kwa ubora na hata nyingine kuwa na matundu baada ya kuondosha rangi ya juu.

Hatua ilipofikia sasa tayari sehemu zote zimezibwa kwa kuweka vyuma vipya(Plates),Kumefungwa Propera Shaft na Vifaa vyake vyote na sasa inasubiriwa Muda wowote kushuka katika Chelezo ili kupachika injini ambazo zipo tayari eneo la Mradi pamoja na Kumalizia kazi ya Kupiga rangi nje na kumalizia kufunga vifaa vilivyobaki kukamilisha sehemu ya ndani.

Pia itakumbukwa kuwa Vitu vinavyofungwa ama kuwekwa katika Meli hii kwa asilimia tisini( 90%)ni vipya.

Meli hii inatarajiwa kuanza safari zake upya kati ya Mwanza na Bukoba mapema mwezi April 2020.