Latest News 14 Dec 2020

News Images

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI AFANYA ZIARA KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Godfrey Kasekenya amefanya ziara Katika Makao Makuu ya Kampuni ya Huduma Za Meli yaliyopo Mwanza ikiwa ni Ziara yake ya kwanza tangu kuteuliwa kwake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuapishwa mapema mwanzoni mwa mwezi wa Kumi na Mbili mwaka huu.

Akiwa katika ofisi za Makao makuu ya Kampuni Jijini Mwanza, Mhe.Kasekenya amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo ndugu Eric Hamissi Pamoja na Menejementi ya wafanyakazi wa Kampuni.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huduma za Meli alimweleza Mhe.Kasekenya historia ya Kampuni hiyo , iliyo ambatana na mafanikio ya sasa baada ya Serikali kuinyanyua tena kwa kuwekeza fedha nyingi za kufufua shughuli za Kampuni .

Serikali ilitenga fedha Shilingi Bilioni 153 kwa ajili ya Miradi ya mwanzo kwa kuanzia katika Ziwa Victoria . Fedha ambayo imetumika katika Ukarabati mkubwa wa Meli ya New Victoria Hapa Kazi tu ambayo Ukarabati wake umetumia shilingi Bilioni 22.7.

Miradi mingine ni Ujenzi wa Chelezo (Sehemu inapo tengenezewa Meli) kwa gharama ya Shilingi Bilioni 36 , Ujenzi wa Meli Mpya ambao utakamilika kwa Shilingi Bilioni 89.76 na Ukarabati wa Meli ya New Butiama Hapa Kazi tu ambao Ulitumia Shilingi Bilioni 4.9

Kampuni ya Huduma za Meli ina Matawi matatu ambayo ni Mwanza,Kyela na Kigoma ambapo hadi sasa ina kampuni inamiliki Meli 14 na boti 1 , Meli 9 zikiwa katika Ziwa Victoria, 3 Ziwa Tanganyika , 2 Ziwa Nyasa huku Boti Moja ikiwa katika Ziwa Tanganyika.

Baada ya Maelezo hayo ya utambulisho, Mhe.Naibu Waziri alifanya Ziara ya Ukaguzi wa Miradi hiyo hasa ambayo imekwisha kamilika kama Meli ya New Victoria Hapa Kazi tu Pamoja na Chelezo ambacho ndicho kina tumika katika Ujenzi wa Meli Mpya .

Pia,metumia nafasi hii kuishukuru kwa usimamizi mzuri wa Miradi, lakini akimpongeza sana Mh.rais kwa maono yake ya kufufua shughuli hizi za usafiri kwa Njia ya Maji na hasa kuifufua Kampuni hii ambayo ilikuwa imepotea.

Ziara hii imefanyika siku moja kabla ya ziara ya waziri mkuu mhe.Khasim Majaliwa ambaye anatarajia kutembelea eneo la Mradi wa Ujenzi wa meli Mpya kujionea maendeleo ya Ujenzi huo,