Latest News 12 Sep 2019

News Images

MAENDELEO UJENZI WA CHELEZO

Sehemu ya Chelezo iliyokamilika ambayo ni ile ya kuunganishia vifaa vinavyounda meli mpya (Block Assembly Area) kama linavyoonekana katika Picha.

Vinasubiriwa sehemu ya vifaa ambavyo vinatarajiwa kuwasili muda wowote eneo la Mradi.

Katika sehemu ya pili ya uzio utakaotumika kutengenezea Slipway(Cofferdam) shughuli inayoendelea sasa ni kutoa maji nje na udongo ulio ndani kisha kupanga mawe tayari kwa hatua inayofuata.

Sehemu ya Kwanza ilikamilika wiki mbili zilizopita ambapo taarifa hizi za sehemu ya pili ya shughuli zinazoendelea kwenye uzio ndizo zinazoendelea kwa sasa.