Latest News 25 Nov 2019

News Images

SHEHENA YA PILI KONTENA 16 VIFAA UJENZI WA MELI MPYA VYAWASILI MWANZA

Shehena ya pili kontena 16 za Vifaa vya Ujenzi wa Meli Mpya vimewasili Mwanza katika eneo la Bandari ya Mwanza Kusini sehemu inapoundwa Meli Mpya yenye jina la MV.Mwanza Hapa Kazi tu

Kuwasili kwa kontena Hizo kunafanya idadi ya kontena kufikia 33 hadi sasa ambapo Shehena ya kwanza ilijumuisha kontena 17 ambapo Vifaa vinakuja kulingana na mahitaji

Kufika kwa Vifaa hivi kunaongeza kasi ya Ujenzi wa Meli hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2021

Mkandarasi wa Ujenzi wa Meli hiyo ni Kampuni ya GAS ENTEC Kutoka nchini Korea ya kusini ikishirikiana na KANGNAM nayo ya korea kusini pamoja na SUMA JKT ya Tanzania