Latest News 30 Nov 2020

News Images

UTEKELEZAJI WA UJENZI WA MELI MPYA

Ujenzi wa Meli Mpya ambao unaendelea kutekelezwa katika Bandari ya Mwanza Kusini Jijini Mwanza umeingia katika hatua mpya ambapo sasa baada ya kukamilika kwa hatua ya kuunganisha sehemu ya chini ya kitako cha Meli, sasa zoezi la kupandisha vipande vikubwa vya vyuma vilivyoungwa pamoja(Blocks) limeanza .Kipande cha kwanza kilicho pandishwa juu kinahusiana na sehemu itakayo kuwa ikibeba mizigo yakiwemo magari makubwa na madogo. Mradi huu ni Mkataba wa Miaka miwili ambapo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2021. Mkandarasi wa Ujenzi wa meli hiyo ni Kampuni ya Gas Entec kutoka Korea ya Kusini ikishirikiana na Kang Nam Cooperation nayo kutoka Korea ya Kusini lakini pia Wazawa Suma Jkt ya Tanzania. Garama ya mradi huu ni Shilingi Bilioni 89.