Latest News 06 Sep 2019

News Images

VIKAO VYA TATHMINI NA UHAKIKI WA MAENDELEO YA MIRADI (MSCL) MWEZI AUGUST 2019

Vikao vya tathmini na uhakiki wa maendeleo ya Miradi inayotekelezwa na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kwa Mwezi August 2019 ambacho ni muendelezo wa vikao vinavyofanyika kila Mwezi tangu kuanza kwa Miradi (Site meeting) vimekamilika kwa timu ya wataalamu kutoka Kampuni ya Huduma za Meli nchini,Wataalamu kutoka Serikalini chini ya Wizara ya Uchukuzi na wadau wengine wa Miradi hiyo kukutana na timu ya wakandarasi wanaotekeleza miradi husika Jijini Mwanza.

Vikao hivi hufanyika kila mwezi na maudhui yake ni kutembelea eneo la utekelezaji miradi ili kuhakiki kile kilichoelekezwa kwenye mikataba na uhalisia wa utekelezaji wake na pia kumuelekeza ama kumuhimiza mkandarasi pale anapokuwa yupo nje ya makubaliano kimkataba

Awamu hii ni kikao cha tano tangu kuanza kwa mradi na kimehudhuriwa na Mkuu wa Jeshi la wanamaji Meja Jenerali Richard Makanzo .

Katika siku ya Pili ya vikao timu nzima ya wataalamu ilialikwa kwa Mh.Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ndugu John Mongella ambaye alipata taarifa za awali za maendeleo ya mradi

Baada ya kupata taarifa, Mh.Mongella ameelekeza katika baadhi ya meeneo kufanyiwa kazi kwa kasi zaidi.

Kwa ujumla Maendeleo ya Miradi yote ipo katika hatua nzuri na inaendana na mpangilio wa makadirio katika makubaliano ya kimkataba.

Kandarasi wanaosimamia miradi hii ni KTMI ya Korea ya Kusini ambayo inahusika na ukarabati wa Meli ya MV.Victoria na MV.Butiama ambayo itakamilika mapema Mwezi March 2020.

Mkandarasi wa Chelezo ni STX Engine kwa kushirikiana na Kampuni ya SAE KYUNG zote kutoka Korea Kusini ambaye anatarajia kukamilisha mradi mapema mwanzoni mwa mwaka 2020 na GAS ENTEC kutoka Korea ya Kusini kwa kusaidiana na SUMA JKT hawa ndio wajenzi wa Meli Mpya ambayo pia itakamilika mwishoni mwa mwaka 2020.

Miradi yote hii inagharimu takribani Kiasi cha Shilingi Bilioni 152 ambapo hadi sasa Serikali imeshalipa Shilingi Bilioni 60.

Fedha zote za miradi hii zimetolewa na Serikali kwa maana ya kwamba Mradi huu hujengwa kwa Pesa za Walipa Kodi wa Tanzania.

Imetolewa na Ofisi ya Habari na Mawasiliano – Kampuni ya Huduma za Meli Nchini