Latest News 21 Dec 2020

News Images

WAZIRI MKUU APONGEZA HATUA ZA MAENDELEO YA UJENZI WA MELI MPYA ZIWA VICTORIA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe.Kassim Majaliwa amepongeza maendeleo ya Mradiwa Ujenzi wa Meli Mpya inayojengwa katika Bandari ya Mwanza Kusini iliyopo Mkoani Mwanza

Meli hiyo ambayo tayari imepewa jina la MV.Mwanza Hapa Kazi tu, itakamilika kwa kiasi cha Shilingi Bilioni 89.76 fedha za ndani,na inataraji kufanya safari zake kati ya Mwanza ,Bukoba Pamoja na bandari Jirani katika Ziwa Victoria na hata nchi jirani zilizopo katika ukanda wa ziwa Victoria.

Katika ziara hiyo Mhe.Waziri Mkuu amepongeza juhudi zinazofanywa na wataalamu hasa watanzania wanaoshiriki katika Ujenzi huo, lakini pia ameipongeza Kampuni ya Huduma za Meli(MSCL) kwa Usimamizi wake thabiti wa Mradi huu Pamoja na Miradi Mingine mitatu ambayo imesha kamilika na tayari ipo kazini kama malengo yalivyo kuwa

Aidha Mhe.Waziri Mkuu amezungumzia suala la ajira zinazotokana na uwepo wa Miradi hii ambapo amefurahi kuona MSCL imetoa kipaumbele kikubwa kwa wazawa wanaoshughulika hasa katika shughuli za ufundi na kupata mafunzo na ujuzi kutoka kwa wageni

’Sehemu hii ni moja kati ya sehemu ambayo kauli mbiu ya Serikali inayosema Hapa Kazi tu inafanya kazi sawasawa kutokana na uhalisia wake kwa watanzania waliopo hapa wanavyo chapa kazi. Leo tusinge kuwa na Shughuli hii ninyi wote mgekuwa wapi?’’ -Anasema Waziri Mkuu

Awali Meneja Mradi wa Ujenzi wa Meli hiyo Mhandisi Vitus Mapunda, alisema ujenzi huo umefikia asilimia 27 ya Ujenzi na mradi huu ni wa mkataba wa miaka miwili kukamilika kwake ambapo unataraji kukamilika katikati ya Mwaka 2021.

Akizungumza baada ya hitimisho la ziara, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amemhakikishia Waziri Mkuu kwamba Mkoa utaendelea kutekeleza maagizo yote yanayotolewa kwa kuyafanyia kazi kama muongozo ulivyo.

Pia ameshukuru Mhe.Rais, Makamu wa rais Pamoja na Serikali kwa Ujumla kwa mipango na mikakati thabiti yautekelezaji wa Miradi inayoendelea hasa iliyopo Mkoani Mwanza kwani itaongeza chachu ya maendeleo ya Mkoa na hatimaye faida kwa watanzania wote.

Mkandarasi wa Ujenzi wa Meli Mpya ni Kampuni ya Gas Entec kutoka nchini Korea ya Kusini ,akishirikiana na Kang Nam Coorperation nayo ya nchini Korea ya Kusini ,Pamoja na SUMA JKT kutoka TanzaniaImetolewa na Ofisi ya Habari na Mawasiliano – Kampuni ya Huduma za Meli